• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

DAS Kanyinda Apongeza Mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nanyumbu

Posted on: June 21st, 2025

Na, Lunanilo Ngela

Katibu Tawala wa Wilaya ya Nanyumbu, Ndg. Juma Said Kanyinda, ameyapongeza mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotekeleza shughuli zake wilayani humo kwa mchango wao mkubwa katika kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika maeneo mbalimbali.

Ndg. Kanyinda alitoa pongezi hizo tarehe Juni 21, 2025, wakati akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu kwenye Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs), lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.

Amesema kuwa mashirika hayo yamekuwa washirika muhimu wa Serikali katika kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali kama vile afya, elimu, kilimo, utunzaji wa mazingira, utawala bora, pamoja na uwezeshaji wa jamii. Aidha, alieleza kuwa mashirika hayo yamechangia katika kutoa ajira kwa wananchi kupitia programu mbalimbali zinazotekelezwa katika maeneo ya vijiji na mitaa.

Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu, Ndg. Philipo Sengela, alisema kuwa jukwaa hilo hutoa fursa kwa mashirika husika kuwasilisha na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli zao. Aliongeza kuwa jumla ya mashirika saba yaliwasilisha taarifa katika jukwaa hilo, yakieleza namna yalivyotekeleza majukumu yao kwa kipindi cha miaka mitano.

Kwa upande wao, baadhi ya viongozi wa mashirika walieleza kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni ukosefu wa rasilimali fedha, jambo linalokwamisha utekelezaji wa baadhi ya mipango yao ya maendeleo. Hata hivyo, walibainisha kuwa pamoja na changamoto hiyo, mashirika yao yameendelea kuwa chachu ya mabadiliko chanya katika jamii.

Mmoja wa washiriki wa jukwaa hilo, Ndg. Dickson Mwichaha kutoka Shirika la Msaada wa Kisheria, alieleza namna shirika hilo lilivyosaidia kutatua migogoro ya kifamilia, hasa migogoro ya ndoa, ikiwa ni pamoja na kusaidia wanaume waliokuwa wakinyanyaswa majumbani, hivyo kuchangia kuimarisha amani katika familia.

Kaulimbiu ya Jukwaa la Mwaka 2025 ni: “Tathmini ya Mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Katika Maendeleo ya Taifa 2020/2021 – 2024/2025.”


Matangazo

  • Matokeo ya Usaili wa Kuandika wa Watunza Kumbukumbu Daraja la II June 28, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • “Nanyumbu: Lango Jipya la Uwekezaji Kusini”

    June 25, 2025
  • DAS Kanyinda Apongeza Mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nanyumbu

    June 21, 2025
  • RC Sawala Aipongeza Nanyumbu kwa Kupata Hati Safi ya CAG

    June 19, 2025
  • FUM Nanyumbu Yavunja Rekodi ya Mapato na Kuandika Historia Mpya ya Miradi

    June 18, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.