Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Benjamin Raphael Masimbo akifungua kikao cha Baraza la Madiwani
Na, Lunanilo Ngela
Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu wamekutana mapema leo Aprili 27, 2023 katika ukumbi wa Halmashauri na kufanya kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Katika Kikao hicho, waheshimiwa Madiwani wamepokea na kujadili taarifa za utendaji kazi katika ngazi ya Kata kwa kipindi cha Mwezi Oktoba - Disemba, 2022
Akizungumza katika Kikao hicho Cha Baraza la Madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri amesema kuwa, ipo miradi mingi ya ujenzi inaendelea kila Kata ikiwa ni juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha maendeleo yanasonga mbele.
Baraza la Madiwani litaendelea kesho Aprili 28, 2023 ambapo miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa ni pamoja na Mapendekezo ya Rasimu ya Sheria Ndogo za Halmashauri za mwaka 2023, Maswali ya papo kwa papo kwa Mwenyekiti wa Halmashauri, kupokea na kujadili taarifa za Kamati za Kudumu za Halmashauri kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi, 2023 ikiwemo taarifa ya Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango, Kamati ya Elimu Afya na Maji, Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira pamoja na Kamati ya Kudhibiti Ukimwi.
Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu
Anwani ya Posta: 246, Masasi
Simu: 0232934112/3
Simu za Mikononi:
Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz
Copyright ©2017 Nanyumbu Distict Council . All rights reserved.