Katika picha ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Benjamin R. Masimbo akifungua mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika mapema leo katika ukumbi wa Halmashauri.
Katika mkutano huo wajumbe wamepokea na kujadili kwa kina Taarifa za Maendeleo kwa kata 17 za halmashauri katika kipindi cha Oktoba – Disemba 2022.
Aidha, Mkutano huo utaendelea kesho tarehe 27/Januari/2023 ikiwa ni siku ya pili ambapo wajumbe watapokea na kujadili Taarifa ya Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango, Kamati ya Elimu, Afya na Maji, Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira pamoja na Kamati ya UKIMWI
Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu
Anwani ya Posta: 246, Masasi
Simu: 0232934112/3
Simu za Mikononi:
Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz
Copyright ©2017 Nanyumbu Distict Council . All rights reserved.