Na, Lunanilo L. Ngela
Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani nchini Tanzania, wagombea ubunge 17 wa Jimbo la Nanyumbu kupitia Chama Cha Mapinduzi waliochukua fomu wamezirejesha ili kuwania ubunge katika uchaguzi huo utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Wagombea hao waliorudisha fomu mpaka leo ni pamoja na Ndg. Hussein Omari, Ndg. Andrew John Napacho, Ndg. Kasembe Haridi Kasembe, Ndg. Ahmed T. Malagano, Ndg. Charles M. Mlaponi, Ndg. Chibwana G. Mlimbe, Ndg. Abdallah B. Nassoro, Ndg. Yahya Ally Mhata, Ndg. Dua W. Nkurua, Ndg. Christopher E. Ndizi, Ndg. Willium Kayombo, Ndg. Vumi Y. Namaha, Ndg. Paul M. Milanzi, Ndg. Dunstani D. Mkapa, Ndg. Joseph R. Mlekoni, Ndg. Wema H. Issa na Ndg. Hassan Issa Chiwanje.
Kaimu Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Nanyumbu Bi. Fatuma Mshihiri amesema kuwa, idadi ya wagombea ubunge kwa mwaka 2020 imeongezeka sana ikilinganishwa na miaka mingine. Ongezeko hilo linatokana na kukua kwa demokrasia ikiwa ni pamoja na hamasa kubwa ya wananchi waliyopata katika kushiriki kikamilifu uchaguzi mkuu.
Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu
Anwani ya Posta: 246, Masasi
Simu: 0232934112/3
Simu za Mikononi:
Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz
Copyright ©2017 Nanyumbu Distict Council . All rights reserved.