• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
    • Maadili ya Msingi
    • Strategies
  • Utawala
    • Muundo
    • Divisheni
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Industry, Trade and Investments
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Planning and Coordination
      • Human Resource Management and Administration
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Natural Resources and Environment Conservation
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Fedha na Biashara
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Information and Communication Technology
      • Government Communication
    • Wards
      • Chipuputa
      • Mangaka
      • Kilimanihewa
      • Sengenya
      • Kamundi
      • Maratani
      • Nandete
      • Nanyumbu
      • Mkonona
      • Masuguru
      • Likokona
      • Michiga
      • Napacho
      • Lumesule
      • Mnanje
      • Mikangaula
      • Nangomba
    • Villages
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Utalii
      • Hifadhi ya Wanyama ya Lukwika Lumesule
      • Daraja la Mtambaswala
      • Sehemu za Kiutamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
    • Elimu
      • Ujenzi wa Vyuo Vikuu
      • Ujenzi wa Vyuo vya Kati
      • Ujenzi wa Shule Binafsi
    • Maeneo ya Viwanda
    • Ujenzi wa Mahoteli
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Ujasiriamali
    • Biashara
    • Ushauri katika Kilimo
    • Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM)
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma

Mifugo 36 yauwawa kikatili kijiji cha Lukula

Posted on: August 14th, 2018

Katibu Tawala wa Wilaya ya Nanyumbu Ndugu Salum A. Palango akizungumza na wananchi wa kijiji cha Lukula katika kikao cha kutatua mgogoro wa wakulima na wafugaji 

Jumla ya mifugo thelathini na sita (36) wakiwemo ng'ombe, mbuzi, kondoo na mbwa wameuwawa kikatili katika kile kilichodaiwa kuwa ni mgogoro kati ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Lukula kata ya Masuguru wilayani Nanyumbu. Siku ya Jumapili ya tarehe 12/Agosti/2018 mfugaji aitwaye Jacksoni Momoita alimjeruhi kwa fimbo mkulima Oscar Tumaini Manduta aliyekuwa akiizuia mifugo kupita karibu na shamba lake hali iliyopelekea wananchi waliokuwa karibu kumvamia mfugaji huyo na kumshushia kipigo. Wananchi hao hawakuishia hapo tuu bali walivamia kambi mbalimbali zenye wafugaji na kuiuwa pamoja na kuijeruhi vibaya mifugo yao.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Nanyumbu Ndugu Salum A. Palango ambaye amemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mh. Moses Joseph Machali akiwa ameongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya amefika kijijini hapo na kufanya mazungumzo na wanakijiji huku akiwaagiza wananchi kuilinda amani. Uongozi wa Wilaya umelaani vikali tabia ya wananchi kujichukulia sheria mkononi na kuwaagiza kutii sheria na kanuni za nchi ili kuilinda na kuidumisha amani. Aidha, vyombo vya Ulinzi na Usalama vinaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Lukula wamesema kuwa wamechoshwa na tabia ya wafugaji kuvamia mashamba ya wakulima na kulisha mifugo yao mara kwa mara. Aidha, wananchi hao wamesema wanashangazwa sana na kitendo cha wafugaji kuyaacha maeneo maalumu waliyotengewa na Serikali kwa ajili ya ufugaji na kwenda kuishi kwenye maeneo ya wakulima na kusababisha migogoro.



Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji Vifaa vya Bayometriki January 23, 2025
  • Tangazo la Nafasi za Kazi August 09, 2024
  • Tangazo la Majina na Mipaka ya Vijiji na Vitongoji September 16, 2024
  • Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 September 26, 2024
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu Yang’ara Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

    May 17, 2025
  • Afisa Mwandikishaji Nanyumbu Awataka Washiriki wa Mafunzo Kuhakikisha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Linatekelezwa kwa Ufanisi

    May 14, 2025
  • DC MAGALA AWAASA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CWT NANYUMBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA VIONGOZI.

    March 19, 2025
  • KAMATI YA MWENGE MKOA WA MTWARA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE NANYUMBU.

    March 17, 2025
  • Ona yote

Video

Kituo cha mabasi Mangaka
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HUDUMA ZA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • RATIBA YA VIKAO VYA HALMASHAURI
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • UTALII NANYUMBU

Tovuti Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Haki Zote Zimehifadhiwa.