Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa ndg Amour Hamad Amour amewataka watendaji kutoa elimu kwa vikundi vya wanawake na Vijana ili viweze kuendelea mbele na kupata faida katika uzalishaji wa mali na kujikwamua kiuchumi. Hayo aliyasema wakati akikagua vikundi vya Wanawake na Vijana na kutaka kutengwa kwa asilimia kidogo kati ya asilimia 5 pesa ambayo inatolewa na halmashauri ili zitumike katika kutoa elimu kwa vijana pamoja na kuibua miradi ambayo itaweza kuwaendeleza kabla ya kupata mikopo ili wajue namna nzuri ya matumizi ya faida wanayoipata kutokana na Mikopo hiyo.
Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu
Postal Address: 246, Masasi
Telephone: 0232934112/3
Mobile:
Email: info@nanyumbu.go.tz
Copyright ©2017 Nanyumbu Distict Council . All rights reserved.