Katibu Tawala wa Wilaya ya Nanyumbu Ndugu Salum A. Palango akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nakopi mara baada ya kukagua maeneo ambako ujenzi wa Ofisi ya Tarafa pamoja na nyumba ya Afisa Tarafa vitajengwa. Katibu Tawala ambaye alipokelewa na Diwani wa Kata ya Napacho Mh. Mary Mchopa amesema kuwa ujenzi wa miundombinu hiyo ya Tarafa unatarajia kukamilika mapema mwaka huu. Aidha, Katibu Tawala ameishukuru sana Serikali inayoongozwa na Rais wa awamu ya tano Mh. Dr John Pombe Magufuli kwa kuratibu na kusimamia ujenzi wa miundombinu mabalimbali vijijini na mijini ili kuharakisha maendeleo.
Diwani wa Kata ya Napacho Mh. Mary Mchopa pamoja na shukrani zake za pekee kwa Serikali pia amewaomba wananchi wa kata ya Napacho kuhakikisha wanashirikiana bega kwa bega katika ujenzi huo wa miundombinu ya Tarafa. Mheshimiwa Diwani pia ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kuupeleka mradi huu katika kata ya Nakopi. Kata ya Nakopi ndio kata pekee kwa sasa ambayo ujenzi huu wa Ofisi ya kisasa na nyumba bora ya Afisa Tarafa vinajengwa. Aidha, baada ya Ujenzi huu Serikali itazigeukia Tarafa zingine.
Wanachi wa tarafa ya Nakopi wametowa shukrani zao za dhati kwa Serikali huku wakiahidi kushirikiana bega kwa bega ili kuhakikisha ujenzi wa miundombinu ya Tarafa unakamilika kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu
Anwani ya Posta: 246, Masasi
Simu: 0232934112/3
Simu za Mikononi:
Barua Pepe: info@nanyumbu.go.tz
Copyright ©2017 Nanyumbu Distict Council . All rights reserved.