• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Complaints |
Nanyumbu District Council
Nanyumbu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • List of Leaders
    • Dira na Dhamira
    • Core Values
    • Stategies
  • Administration
    • Muundo
    • Idara
      • Water
      • Kilimo
      • Finance and Accountants
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Nanyumbu yapewa zaidi ya Bilioni 80 kutekeleza mradi wa maji Mto Ruvuma

Posted on: October 26th, 2020

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Nanyumbu


 Na, Lunanilo L. Ngela

Katika mkutano uliofanyika viwanja vya mabasi Mjini Mangaka, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amewaeleza wananchi wa Nanyumbu juu ya Mradi mkubwa wa maji wa mto Ruvuma uliotengewa zaidi ya shilingi Bilioni 80 ili kusambaza maji wilayani humo.

Mradi huo ambao ni utekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi unatarajia kuanza mapema mwezi Novemba na tayari mkandarasi amekwishapatikana na usanifu wa mradi umekamilika.

Waziri Mkuu amesema nia ya Serikali ni kumtua mwanamke ndoo. Aidha, ameongeza kuwa kampeni ya kumtua mwanamke ndoo haitaishia vijijini na mijini tuu bali sasa inakwenda mpaka ngazi ya vitongoji na visiwa.

Akizungumzia suala la miundombinu ya usafiri Mhe. Kassim Majaliwa amesema katika kipindi cha 2020-2025 Serikali itajenga reli ya kisasa toka Mtwara mpaka Mbamba Bay Ruvuma ikipitia wilayani Nanyumbu. Aidha, Barabara ya Nanyumbu - Nachingwea mpaka Morogoro pamoja na barabara za lami mjini Mangaka zitajengwa katika kipindi hicho ili kuendelea kurahisisha huduma za usafiri.

Waziri Mkuu akizungumzia suala ka korosho amesema Serikali itaendelea kuhakikisha wakulima wanauza korosho zao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani ili kumsaidia mkulima kupata bei nzuri na kutodhurumiwa na wafanyabiashara. Aidha, ametoa maelekezo kuwa mkulima au mfanyabiashara asikatwe unyaufu kwani korosho inanyauka baada ya miezi sita.

Akizunguzia suala la Elimu amesema katika kipindi cha 2020-2025 Serikali itajenga mabweni kwa shule zote za sekondari za Serikali ili kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira tulivu.

Ndugu Majaliwa Kassim Majaliwa (MNEC) ameomba kura za ndiyo kwa mgombea wa kiti cha urais Ndg. John Pombe Magufuli kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi pamoja na wagombea ubunge na udiwani wa chama hicho. Aidha, Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani utakaofanyika Tarehe 28/10/2020 nchini pote na hivyo amewakumbusha wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura


Matangazo

  • FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA KWA MWAKA WA MASOMO 2021/2021 SHULE ZA SEKONDARI WILAYA YA NANYUMBU December 20, 2020
  • Ona yote

Habari Mpya

  • Nanyumbu yanunua meza na viti kwa ajili ya wanafunzi wa sekondari watakaoanza Januari Mwakani

    December 10, 2020
  • Nanyumbu yapewa zaidi ya Bilioni 80 kutekeleza mradi wa maji Mto Ruvuma

    October 26, 2020
  • Wakulima Nanyumbu wahamasishwa kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya

    September 18, 2020
  • Nanyumbu kujenga mnada wa mifugo

    September 16, 2020
  • Ona yote

Video

Utalii wa ndani Nanyumbu
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • miongozo

Tovuti Mashuhuri

  • Public Service Management
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu

    Anwani ya Posta: 246, Masasi

    Simu: 0232934112/3

    Simu za Mikononi:

    Barua Pepe: info@nanyumbudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2017 Nanyumbu Distict Council . All rights reserved.